WOKOVU - KAZI KUU YA MUNGU
UTANGULIZI
Kila anayetaka kwenda mbinguni na kujenga mahusiano mazuri na Mungu, lazima afahamu kwa usahihi yale ambayo Biblia inafundisha kuhusu wokovu. Ufahamu sahihi wa elimu ya wokovu ni muhimu kwa kila anayetumaini kuokolewa kwa sababu ni msingi wa imani ya kweli. Mtu akiukosa ufahamu sahihi wa wokovu, anaweza kufikiri kwamba ameokolewa, kumbe si kweli, bali amejidanganya. Atajutia siku atakaposimama mbele ya Kristo na kuambiwa, “Sikukujua, ondoka kwangu”. Pia, mbaya zaidi, anaweza kuwashuhudia watu Injili isiyo ya kweli hata na wao pia wakatupwa motoni pamoja naye. Shida nyingine inayosababishwa na kutoelewa wokovu kwa njia iliyo sahihi ni kwamba inaweza kusababisha mtu aliyeokoka kweli kuwa na mashaka juu ya wokovu wake na kukosa amani na raha ambazo ni matunda ya wokovu wa kweli.
Katika somo hili tutachunguza Biblia inavyofundisha kuhusu wokovu ili kila mmoja wetu awe na ufahamu sahihi wa wokovu. Ufahamu sahihi wa wokovu ni msingi muhimu wa maisha ya Kikristo. Ili Mkristo aweze kuishi kama anavyopaswa, anahitaji kuyajua yale yaliyofanyika alipookolewa na ajue uwezo alio nao katika kuishi maisha mapya. Tutajifunza jinsi wokovu unavyomletea Mkristo maisha haya mapya.
Lakini pia, kwa sababu watu wengine wameyachanganya mafundisho ya wokovu, tutayachunguza mafundisho ya uongo kuhusu wokovu pia. Kwa mfano hali ya kutegemea matendo mema kwa wokovu au utegemezi katika kifo cha Yesu pamoja na ubatizo. Tutaona kwa nini mafundisho haya ni ya uongo na kwa nini mafundisho haya hayawezi kumwokoa mtu ye yote.
Kitabu hiki kinagawanyika katika sehemu kuu mbili. Katika sehemu ya kwanza tutajifunza yale ambayo mwenye dhambi anapaswa kuyajua na kuyaamini ili aokolewe. Katika sehemu ya pili tutajifunza jinsi wokovu unavyokuwa msingi wa maisha ya Kikristo.
Kabla hatujaanza, tufafanue maneno na mawazo mengine yanayohusu wokovu. Ni muhimu kufanya zoezi hilo kwa sababu maneno mengine yana maana zaidi ya moja na hata uelewa wa watu kuhusu maana ya maneno mengine ni tofauti.
Kwanza, wewe mwenyewe ufafanue jinsi unavyoelewa maneno haya:
Jibu maswali yafuatayo kwa kuweka “x” kwenye nafasi ya jibu lililo sahihi.
Kufuatana na ufafanuzi wako wa “Mkristo”, Wakristo wangapi wameokolewa?
____Wote____Karibu Wote____Baadhi____Hakuna
Kufuatana na ufafanuzi wako wa “Muumini”, Waumini wangapi wameokolewa?

Kufuatana na ufafanuzi wako wa “Mshirika wa Kanisa”, washirika wangapi wameokolewa?

Kufuatana na ufafanuzi wako wa “Mwenye kuhudhuria kanisani”, wangapi kati ya hawa wameokolewa?

Kuna njia zaidi ya moja ya kufafanua maneno hayo. Lakini utakapoona maneno hayo katika kitabu hiki ujue ninatumia maana zifuatazo:
Je, ufafanuzi au matumizi yako ya maneno haya yanaendana na maana ya maneno haya katika kitabu hiki? Utakapoendelea kusoma kitabu hiki, kumbuka maana ninayotumia wakati ninaandika ili uweze kuelewa ujumbe wa kitabu hicho.
Tuangalie zaidi neno “Wokovu”. Maneno muhimu katika ufafanuzi wangu ni “ushirikiano” na “kurejeza”. Watu wengine wanafikiri Mungu anataka kutuokoa kwa sababu ya thamani tuliyo nayo sisi. Lakini katika kitabu hiki tutaonesha jinsi wokovu unahusu zaidi jinsi Mungu anavyostahili kuabudiwa. Yaani wokovu unahusu thamani ya Mungu kuliko thamani ya wanadamu.
Maneno “ushirikiano na Mungu” yanaonesha kusudi la wokovu. Mungu aliumba wanadamu waishi wakiwa na uhusiano naye milele. Ndiyo sababu anaokoa watu. Kuwemo katika ushirika na Mungu kunaanza siku ya kwanza mtu anapookolewa, hakusubiri mtu afike mbinguni. Tutajifunza maana ya kuwa na ushirika na Mungu na jinsi tokeo moja la kuokoka ni hamu ya kuwa na ushirikiano huo.
Mwishoni, neno “kurejeza” linatuonesha kwamba kulikuwa wakati wanadamu walikuwa katika uhusiano mzuri na Mungu, lakini ushirikiano ule ulivunjwa. Tutaona jinsi uhusiano ule ulivyoharibiwa na jinsi Mungu alivyoshughulika ili aurejeze. Pia tutaona jinsi uhusiano huu uliorejezwa, utakavyodumu milele.

- Mkristo
- Muumini
- Mshirika wa Kanisa
- Mwenye kuhudhuria Kanisani
- Wokovu
Jibu maswali yafuatayo kwa kuweka “x” kwenye nafasi ya jibu lililo sahihi.
Kufuatana na ufafanuzi wako wa “Mkristo”, Wakristo wangapi wameokolewa?
____Wote____Karibu Wote____Baadhi____Hakuna
Kufuatana na ufafanuzi wako wa “Muumini”, Waumini wangapi wameokolewa?
____Wote____Karibu Wote____Baadhi____Hakuna
Kufuatana na ufafanuzi wako wa “Mshirika wa Kanisa”, washirika wangapi wameokolewa?
____Wote____Karibu Wote____Baadhi____Hakuna
Kufuatana na ufafanuzi wako wa “Mwenye kuhudhuria kanisani”, wangapi kati ya hawa wameokolewa?
____Wote____Karibu Wote____Baadhi____Hakuna
Kuna njia zaidi ya moja ya kufafanua maneno hayo. Lakini utakapoona maneno hayo katika kitabu hiki ujue ninatumia maana zifuatazo:
- Mkristo – Ni mtu aliyeokolewa kweli.
- Muumini - Ni mtu aliyeokolewa kweli.
- Mshirika wa Kanisa – Ni mtu aliyepokelewa katika tawi la Kanisa ambaye labda ameokolewa au labda hajaokolewa.
- Mwenye kuhudhuria Kanisani – Ni mtu anayehudhuria tu. Pengine ameokoka, pengine hajaokoka. Pengine ni mshirika na pengine siyo mshirika.
- Wokovu – Ni kurejezwa na kupatanishwa na Mungu ili mtu awe na uhusiano na ushirikiano na Mungu.