GMI PUBLICATIONS
GMI PUBLICATIONS
  • Home
  • Kupakua Vitabu
  • Kuhusu Sisi
  • Mawasiliano
  • Home
  • Kupakua Vitabu
  • Kuhusu Sisi
  • Mawasiliano

WOKOVU - KAZI KUU YA MUNGU

- 6 -

Wokovu ni Nini?

Katika mwanzo wa kitabu hiki tulieleza wokovu ni kurejezwa au kupatanishwa katika uhusiano wetu na Mungu. Sasa tufafanue zaidi maana yetu tukiunganisha yale tuliyojifunza hadi sasa:

Wokovu ni kazi ya Mungu kumwokoa mwenye dhambi kutoka katika utawala wa Shetani na adhabu ya dhambi na kutengeneza uhusiano na ushirikiano kati ya mwenye dhambi na Mungu na kumweka chini ya utawala wa Mungu.

Kwa ufafanuzi zaidi wokovu ni kuokolewa kutoka hali moja hadi hali nyingine mpya tunayopewa na Mungu.
 
KUTOKA                                 HADI

Mfu Kiroho                              Hai Kiroho
Utawala wa Shetani             Utawala wa Mungu
Utumwa wa dhambi            Utumwa wa Mungu
Utumwa wa Utu wa Kale    Kutawala Utu wa Kale
Ghadhabu ya Mungu           Upendo wa Mungu
Hukumu ya Mungu               Kibali cha Mungu
Laana ya Mungu                    Baraka ya Mungu
Hali ya Uchafu                       Hali ya Usafi
Kutenganishwa na Kristo     Kuunganishwa na Kristo
Kutokuwa na Tumaini           Kuwa na Tumaini
Kuwa mwenye Hatia             Kuwa Mwenye Haki
Adui ya Mungu                       Rafiki ya Mungu
Picture
Mchoro #8 – Mtu wa kushoto bado hajaokolewa. Bado yuko chini ya utawala wa Shetani na dhambi. Mtu wa kulia ameokolewa na yuko katika uhusiano mzuri na Mungu.
Tunaona katika mchoro #8 kwamba:


  • Wokovu siyo kujitahidi kumpendeza Mungu
  • Wokovu siyo kuokoa mtu kutoka utawala wa Shetani na dhambi tu ili ajitawale
  • Wokovu siyo kukoa mtu asiadhibiwe tu

Yaani, wokovu ni kutoka katika hali fulani ili tupewe hali nyingine mpya. Jambo muhimu katika hali mpya ile ni uhusiano wetu na Mungu. Uhusiano wa kuwa chini yake na uhusiano wa kushirikiana naye katika upendo, imani, na ibada. Katika sehemu ya pili ya kitabu hiki tunaangalia zaidi maana ya kuwa katika uhusiano na Mungu.

RUDI KWENYE ORODHA YA SURA
sura ya 7
Proudly powered by Weebly