WOKOVU - KAZI KUU YA MUNGU
- 20 -
Kunamtokea nini Mtu Anapookolewa?
Warumi 6:3-4 – “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.”
Waefeso 2:10 – “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.”
Matokeo ya wokovu katika maisha ya Mkristo ni kuishi maisha mapya ya matendo mema. Ni namna gani Mkristo ataweza kuishi maisha haya mapya? Mungu alipotuokoa, alitupa uwezo wa kuishi maisha haya mapya (2 Pet 1:3). Tuyarudie na kukumbuka mambo Mungu aliyotujalia alipotuokoa:
Mungu ametuwezesha kuishi maisha yanayompendeza yeye
Tunaona kwamba kupitia mambo yaliyo hapo juu, wakati Mungu alipotuokoa, kweli alitujalia uwezo wote wa kuishi maisha mapya ya kufanya matendo mema. Ametuweka huru na mamlaka ya Shetani na dhambi. Kwa hiyo hatupaswi kufanya dhambi tena. Ametupatia hamu mpya ya kuyafuata maagizo na mapenzi yake. Kupitia Roho Mtakatifu na kuungwa na Kristo tumepewa uwezo wa kuishi maisha matakatifu na kuyafanya matendo mema yanayompendeza na kumpa utukufu.
Maana kwetu
Basi, wajibu wetu ni nini? Ni kujua mambo haya, kuyaamini mambo haya na kuishi kufuatana na yale tunayoamini. Ndivyo jinsi wokovu wetu unavyotuwezesha kuishi maisha mapya.
Tuishi sasa kwa uwezo tulio nao kutoka kwa Mungu kwa ajili ya utukufu wake.

- Mungu ametukomboa kutoka katika mamlaka ya Shetani na dhambi ili tuishi maisha yasiyo na dhambi kwa sababu hatutawaliwi na Shetani wala dhambi tena.
- Mungu ameturudisha chini ya utawala wake kama watumwa wake ili tumtii Mungu na kuishi maisha yanayolingana na mapenzi yake.
- Mungu ametuzaa mara ya pili ili tuwe na hamu mpya ya kumpendeza Mungu kuliko mambo yote.
- Mungu ametupatia Roho Mtakatifu ili tuwe na uwezo wa kuishi maisha matakatifu.
- Mungu ametuunga na Kristo ili tuwezeshwe kuzaa tunda la kiroho.