GMI PUBLICATIONS
GMI PUBLICATIONS
  • Home
  • Kupakua Vitabu
  • Kuhusu Sisi
  • Mawasiliano
  • Home
  • Kupakua Vitabu
  • Kuhusu Sisi
  • Mawasiliano

WOKOVU - KAZI KUU YA MUNGU

- 19 -

Uzima wa Milele Unadumu Muda Gani?

Haiwezekani kuupoteza wokovu uliotolewa na Mungu

Watu wengine wanadhani kwamba wataupoteza wokovu wao wakitenda dhambi. Lakini, Biblia inafundisha wazi kwamba wokovu ni zawadi ya milele na hatuwezi kuipoteza zawadi hiyo. Baadhi ya vifungu vinavyothibitisha umilele wa wokovu ni kama vifuatavyo: Yoh 3:16,36; Yoh 6:37; Yoh 10:28; Rum 8:1; Rum 8:35-39; Efe 4:30; Ebr 10:10-14.

Kama tunaweza kuupoteza wokovu ina maana Yesu hajafa kwa ajili ya dhambi zetu zote (ndiyo kusema kifo cha Yesu kina mapungufu)

Tumeona kwamba wakati Yesu alipokufa msalabani, alichukua dhambi zetu zote. Alijitoa mara moja tu kama dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu zote. Aliadhibiwa kwa ajili ya dhambi zetu zote. Aliziondoa dhambi zetu zote. Alitusafisha dhambi zetu zote ili tusamehewe dhambi zetu zote. Ndiyo sababu tunasoma katika Waebrania 10:12-14 kwamba kupitia dhabihu yake moja msalabani, ameshawakamilisha hata milele wale ambao wameokolewa. Kusema kwamba mtu anaweza kupotea tena, ni kusema kwamba mtu yule ataadhibiwa kwa ajili ya baadhi ya dhambi zake. Tukisema kwamba ataadhibiwa kwa ajili ya baadhi ya dhambi zake, tunasema kwamba dhabihu ya Yesu haikutosha kutusamehe dhambi zetu zote. Kama kifo cha Yesu hakikufaa kutusamehe dhambi zote, Yesu alikufa bure na hakuna wokovu.
 
 Mungu alilitumia neno milele kwa kuwa alimaanisha milele

Mungu aliamua kuiita zawadi tunayopokea tunapomwamini Yesu nini? Uzima wa milele. Neno “milele” linamaanisha nini? Uzima usio na mwisho; unaodumu milele. Kama mtu angeweza kupoteza wokovu wake, ingekuwa bora kwa Mungu kuita zawadi yake “uzima wa muda” au “uzima mpaka utakapotenda dhambi” au “uzima mpaka _____?_____.” Asingeita zawadi yake “uzima wa milele”. Kuona kwamba Mungu alichagua kuiita zawadi yake uzima wa milele, tunaweza kusema bila shaka kwamba uzima tunaopokea tunapookolewa utadumu milele. Kama mtu anaupokea uzima wa milele kutoka kwa Mungu halafu baadaye anaukuta uzima huo unaisha ina maana Mungu amekuwa mwongo. Mungu siyo mwongo hivyo akisema milele, ujue ni milele.


RUDI KWENYE ORODHA YA SURA
sura ya 20
Proudly powered by Weebly