WOKOVU - KAZI KUU YA MUNGU
- 11 -
Nifanye Nini Nipate Kuokoka?
Mtu akitaka kuokolewa, afanye nini? Watu wengine wanasema lazima mtu huyu aache kutenda dhambi, wengine wanasema afanye matendo mema au atii mafundisho ya Yesu. Tumeshaona katika kitabu hiki kwamba hakuna atakayeokolewa kwa njia ya kuacha dhambi wala kwa kutenda matendo mema.
Biblia inatoa jibu moja tu kwa ajili ya swali hilo: Mwamini Bwana Yesu Kristo (Mdo 16:31; Yn 3:15, 16, 36; 5:24; 6:40, 47; 20:31; Mdo 10:43; Rum 1:10; 4:23-34; 10:9; 1 Tim 1:16; 1 Yn 5:1, 13).
Matendo 16:31 - “Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.”
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”
1 Timotheo 1:16 - “Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele.”
Kumwanini Yesu kuna maana gani? Ukimwambia mtu kumwamini Yesu, ni mambo gani ambayo unataka aamini? Andika jibu lako hapo chini (Lakini usitumie jibu la “kumpokea Yesu,” “kumkubali Yesu,” au maneno mengine yanayofanana na “kuamini”).
Maana ya kumwamini Yesu ni:
Baadaye katika sura hii tutafafanua maana ya kumwamini Yesu lakini kwanza tuangalie mawazo mabaya au ya uongo.
Je, kila anayemwamini Yesu ataokolewa? Labda utashangaa jibu letu; jibu letu ni hapana. Biblia inafundisha kwamba watakuwepo watu wengi wanaosema wamemwamini Yesu lakini wengine kati ya hawa watakuwa hawajaokoka. Wenyewe ni Wakristo kwa jina tu, siyo Wakristo wa kweli. Siku ya mwisho, hawa watatambulishwa na wataadhibiwa (Mt 7:21-23).
Inawezekanaje mtu amwamini Yesu na asiokoke? Tuangalie njia tatu.
Watu wanaweza kumwamini Yesu bila kuokolewa wakiamini bila kuelewa maana ya kweli ya kumwanini Yesu
Watu wakiambiwa kumwamini Yesu bila kuelezwa ni mambo gani ambayo wanapaswa kuamini kuhusu Yesu, pengine wataamini mambo mengine yasiyoweza kuwaokoa. Labda yale watakayoamini yatakuwa habari iliyo kweli au ya uongo. Hata kama ni kweli, haitawasaidia kuokoka kama siyo habari husika. Kwa mfano, ikiwa mtu atafikiri maana ya kumwamini Yesu ni kutii mafundisho yake, je, imani hiyo itamwokoa? Hapana. Mwingine akifikiri maana ya kumwanini Yesu ni kuhudhuria kanisani, je, imani hiyo itamwokoa? Hapana. Ikiwa mtu atafikiri maana ya kumwamini Yesu ni kuacha kutenda dhambi, je, imani hiyo itamwokoa? Hapana. Ili mtu aokolewe, lazima aelewe maana halisi ya kumwanini Yesu inayookoa.
Watu wanaweza kumwamini Yesu bila kuokolewa wakimwamini lakini pia wanategemea kitu kingine kuchangia wokovu wao pia
Mtu akimwamini Yesu na wakati huo huo anaamini kitu kingine cha pili kama matendo mema, ubatizo, kutii amri kumi n.k. mtu huyu hajaokolewa. Vilevile kama mtu atamwamini Yesu ili apate msamaha kwa ajili ya dhambi alizozitenda kabla hajamwanini Yesu lakini anategemea kuungama njiani kwa ajili ya dhambi zote atakazozitenda baada ya kumwamini Yesu, huyu naye hajaokolewa. Kwa nini? Kwa sababu Biblia inafundisha imani inayookoa ni imani inayomlenga Yesu peke yake. Kwa maneno mengine, ni lazima mtu aweke imani yake yote katika Yesu ili asamehewe dhambi zake. Mtu anayemwanini Yesu lakini pia anaamini kitu kingine kiasi fulani, hajaweka imani yake yote katika Yesu. Akimwamini Yesu na pia sehemu fulani ubatizo, akimwamini Yesu na pia matendo mema, akimwamini Yesu na pia kutii amri za Mungu, ina maana hajamwanini Yesu asilimia yote peke yake.
Kwa mfano, Mtu akiomba kikombe cha maji kwako na unamletea kikombe cha chai ukisema, “Haya ni maji yakichanganywa na majani ya chai kidogo.” Je, mtu huyu atakubali ni maji? Hapana. Maji yaliyochanganywa na majani ya chai bado ni maji? Hapana, sasa yanaitwa chai.
Vivyo hivyo na imani. Tukichanganya imani katika Kristo pamoja na imani katika kitu kingine kama matendo mema au mahudhurio kanisani, imani hiyo siyo imani inayookoa tena kwa kuwa siyo imani katika Kristo tu. Maji halisi ni maji safi au maji tupu. Imani halisi inayookoa ni imani katika Kristo peke yake isiyochanganywa na cho chote kingine.
Yesu alipokuwa msalabani alisema, “Imekwisha!” (Yn 19:30). Alikuwa na maana gani alipotamka hivyo? Alikuwa na maana kwamba kifo chake msalabani kilitosha katika kulipia adhabu ya dhambi zote na hakuna kitu kingine kilichohitajika ili watu wapate kuokolewa. Malipo ya mshahara wa dhambi yaliisha. Watu wakisema ni lazima kumwamini Yesu pamoja na kitu kingine ili tuokolewe, ina maana kifo cha Yesu hakikutosha na hakikumaliza deni la dhambi. Kusema hivyo ni kupuuza kazi kubwa ambayo Yesu alifanya msalabani kwa kuwa kweli kweli kifo chake kilitosha na hakuna haja ya kuongeza cho chote kingine.
Mtu anaposema njia ya kuokolewa ni kumwamini Yesu na pia kuongeza kitu kingine, mtu huyu anabadilisha Injili ya Yesu. Katika Wagalatia, mtume Paulo aliwaonya wasibadilishe Injili ya Yesu.
Wagalatia 1:6-9 – “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.”
Katika kanisa la Galatia wengine walianza kuhubiri kwamba Injili ya Yesu haitoshi. Walitaka kulazimisha Wakristo kuongeza utiifu wa sheria ya Musa pamoja na tendo la kutahiriwa. Lakini Paulo anahoji kuongeza cho chote kingine ni kufanya kifo cha Yesu kuwa bure, tena anasema ni ishara ya kukataa neema ya Mungu inayopatikana katika kumwamini Yesu.
Wagalatia 2:18-21 – “Lakini ikiwa ninajenga tena kile nilichokwisha bomoa, basi nahakikisha kwamba mimi ni mhalifu. Maana, kuhusu sheria hiyo, mimi nimekufa; sheria yenyewe iliniua, nipate kuishi kwa ajili ya Mungu. Mimi nimeuawa pamoja na Kristo msalabani, na sasa naishi, lakini si mimi tena, bali Kristo anaishi ndani yangu. Maisha haya ninayoishi sasa naishi kwa imani, imani katika Mwana wa Mungu aliyenipenda hata akayatoa maisha yake kwa ajili yangu. Sipendi kuikataa neema ya Mungu. Kama mtu hufanywa mwadilifu kwa njia ya sheria, basi, Kristo alikufa bure!”
Watu wanaweza kumwamini Yesu bila kuokolewa wakiamini bila kutubu
Kutubu ni lazima katika kumwamini Yesu kwa sababu Mungu aliagiza watu wote kutubu (Mdo 17:30). Ikiwa mtu atasema amemwamini Yesu lakini hajatubu, kumbe hajatimiza maana kamili ya kumwamini Yesu ili aokolewe. Tendo la kutubu linalohusika katika kumwamini Yesu linafafanuliwa katika Neno la Mungu. Kwa kuwa mawazo ya namna ya kufafanua neno hilo ni mengi, lazima tulitegemee Neno la Mungu ili tuelewe vizuri jinsi toba inavyohusika katika wokovu. Baadaye katika kitabu hiki tutafundisha kuhusu maana ya toba katika Neno la Mungu.
Kumwamini Yesu Kristo kuna maana gani?
Biblia ni wazi kwamba wokovu unapatikana katika kumwamini Yesu Kristo tu. Yesu mwenyewe alisema:
Yohana 14:6 - “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”
Lakini kumwamini Yesu ina maana gani? Kuamini ni hali ya kuwa na imani. Kumwamini Yesu ni kumtegemea. Ni kukubali hujiwezi na ni kukubali kumtegemea Yesu kwa kuwa unaamini yeye anaweza. Ni kuamini mambo fulani kuhusu jinsi Yesu alivyo na pia mambo fulani kuhusu kazi aliyofanya, anayofanya, na atakayofanya kwa ajili yetu. Ingawa kuna mambo mengi, yaliyo muhimu zaidi ni kwamba Yesu ni Mungu, Mwokozi, na Bwana.
Kumwamini Yesu ni kuamini Yesu ni Mungu
Kwanza, ni lazima mtu anayetaka kuokoka ajue na kuamini kwamba Yesu ni Mungu (Mk 14:61-62). Biblia inasema imani ya kweli inatakiwa kuamini kwamba Yesu ni Mungu.
Yohana 20:21- “Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.”
Yesu siyo Nabii tu, Yesu ni Mungu wa milele aliyezaliwa kama mwanadamu. Asingekuwa Mungu asingeweza kuishi maisha bila dhambi ili aweze kufa kwa ajili ya dhambi za wengine.
Kumwamini Yesu ni kuamini yeye ni Mwokozi
Pili, ni lazima mtu anayetaka kuokoka ajue na kuamini kwamba Yesu ni mwokozi.
2 Petro 3:18 - “Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.”
Ina maana gani kuwa mwokozi? Mwokozi ni yule anayeokoa mwingine kutoka uovu au hatari. Tuangalie mifano miwili ili tuelewe vizuri maana ya Yesu kuwa mwokozi. Katika mfano wa kwanza, Danieli yumo gerezani na lazima alipe faini ya 50,000 tsh ili atoke gerezani. Rafiki wa Danieli, Isaka, anakubali kulipa 25,000 tsh ili Danieli atoke gerezani. Je, 25,000 tsh zinatosha ili Danieli atoke? Hapana. Je, Danieli angemwita Isaka kuwa mwokozi wake? Hapana. Kulipa sehemu ya faini kusingemfanya Isaka kuwa mwokozi kwa sababu kwa njia hiyo Danieli hataokolewa na hali ya kufungwa.
Katika mfano wa pili Danieli bado yumo gerezani mpaka alipe 50,000 tsh. Mjomba wake anakubli kumlipia zote 50,000 tsh na hivyo Danieli anatoka gerezani. Je, Danieli angemwita mjomba wake mwokozi? Ndiyo, kwa sababu mjomba wake alimwokoa na hali ya kifungo.
Watu wengi wanamwita Yesu mwokozi bila kuamini Yesu aliwaokoa na adhabu ya dhambi zao. Ingawa wanamwita mwokozi, ukweli ni kwamba hawamwamini kama mwokozi. Kama Yesu hakutuokoa na dhambi zetu zote—tulizotenda, tunazotenda, na tutakazotenda—basi Yesu siyo mwokozi wetu.
Lakini ukweli ni kwamba Yesu ni mwokozi wetu. Kwa nini tunaweza kumwita mwokozi? Kwa sababu wakati alipokufa msalabani alibeba dhambi zetu zote na Mungu alimwadhibu kwa ajili ya dhambi zetu zote. Kwa kuwa aliadhibiwa kwa ajili yetu, ametuokoa sisi na matokeo yake ni kwamba hatutaadhibiwa sisi wenyewe.
Ili mtu amwamini Yesu kama mwokozi wa maisha yake ni lazima aweke imani yake yote katika Yesu na kazi aliyoifanya msalabani. Ni lazima aamini kifo cha Yesu kilimaliza deni au mshahara wa dhambi unaodaiwa na Mungu kwa ajili ya dhambi zake. Kuamini Yesu alikufa kwa ajili ya baadhi ya dhambi zake ina maana bado mtu huyu ataadhibiwa kwa ajili ya dhambi zilizobaki. Lakini anayeamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zake zote ataokolewa kwa kuwa ataamini kweli kweli Yesu ni mwokozi wake.
Kumwamini Yesu ni kuamini Yesu ni Bwana
Tatu ni lazima mtu anayetaka kuokoka ajue na kuamini Yesu ni Bwana:
Warumi 10:9 - “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.” (angalia pia Mdo 2:36)
Neno “Bwana” lina maana gani? Maana yake ni kuwa mtawala. Biblia inasema ni lazima mtu aamini Yesu ni Bwana wa maisha yake ili aokoke (Rum 10). Maana yake nini? Mtu anayeokolewa na Yesu, lazima aamini kwamba Yesu ni Bwana na mtawala wa maisha yake. Ni kusema mtu huyu anaamini anapaswa kumpa Yesu nafasi ya kwanza katika maisha yake na kwamba anapaswa kumtumikia Yesu na moyo wake wote akiishi kutimiza mapenzi ya Yesu.
Ni suala la imani na siyo matendo wala utiifu. Wakati mtu anapookoka anamwamini Yesu kuwa Bwana. Ndiyo kusema anakubali ukuu wa Yesu na haki ya Yesu kutawala maisha yake. Mtu akiamini hivyo pamoja na kumwamini Yesu kama mwokozi, mtu huyu ataokolewa. Baada ya kuokoka, imani hiyo ya kwamba Yesu ni Bwana, italeta mabadiliko katika maisha ya mtu huyo. Kabla hatujaokolewa, tuliishi kwa kufuata mapenzi yetu sisi wenyewe. Baada ya kuokolewa tunapaswa kuacha kufuata mapenzi yetu na badala yake tunapaswa kufuata mapenzi ya Yesu na kuishi kwa ajili yake. Ni hali itakayoonekana kwa wote, tena ni ishara ya kwamba mtu ameokoka. Kufanya mabadiliko katika maisa yetu ili tuwe watiifu wa Yesu hakutuokoi bali ni matokeo ya kawaida ndani ya maisha ya mtu aliyeokoka na kuamini Yesu ni Bwana.
Kumwamini Yesu ni kumtegemea
Tunamaanisha nini tunaposema kwamba anayeiamini Injili au kumwamini Kristo anapata wokovu? Mtu akikubali kwamba Injili ni kweli, je, tayari ameokoka? Hapana. Akikubali Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu na kufufuka tena, je, amepata wokovu? Hapana. Kukubali kwamba Yesu ni Mungu kunatosha kumfanya mtu aokoke? Hapana. Hizo zote ni habari zinazomhusu Yesu. Kuna habari nyingi za Yesu ambazo mtu anaweza kujua, na kukubali ni kweli, bila mtu huyu kuokoka. Kwa mfano, Yesu alifanya miujiza, Yesu alipaa kwenda mbinguni, Yesu alizaliwa duniani, n.k. Kukubali siyo imani kamili. Kitu gani kinakosekana katika kukubali habari kuwa kweli? Kumtegemea Kristo. Kuamini siyo kukubali maarifa katika akili zetu bali ni kuyaamini maarifa yale katika mioyo yetu hadi tunapokuwa tayari kumtegemea Yesu kama mwokozi wetu.
Kumwamini Yesu ni kumtegemea Yesu akiwa Mungu.
Ni kutegemea Yesu ana uwezo wa kutuokoa kwa sababu yeye ni Mungu. Ni kutegemea Yesu ni mwenye nguvu zote na ana uwezo kutuokoa kwa sababu yeye ni Mungu. Ni kutegemea Yesu ni mwenye maarifa yote na anajua namna gani ya kutuokoa kwa sababu yeye ni Mungu. Ni kutegemea Yesu ni mwenye maarifa yote na hivyo anajua siku zetu zijazo na anajua ni wakati gani atatupeleka mbinguni. Ni kutegemea Yesu aliye Mungu habadiliki na kwa sababu hiyo ahadi zake hazitabadilika. Ni kutegemea Yesu anaposema ametuokoa ni jambo linaloaminika leo na kesho na milele.
Kumwamini Yesu ni kutegemea Yesu ni Mwokozi.
Ni kuacha kujaribu kujiokoa. Ni kuacha kutafuta njia nyingine ya kuokolewa. Ni kuamini wokovu tunao kwa sababu tunaamini maneno ya Yesu na pia tunaamini kazi aliyotufanyia, anayotufanyia, na atakayotufanyia. Kazi zake ni nyingi kwa niaba yetu katika kuwa mwokozi wetu. Tunategemea kazi hizo zote. Tunategemea alilipa mshahara wa dhambi zetu na hivyo tunapumzika katika yeye bila kuhangaika. Tunategemea alishinda mauti alipofanya kazi ya kufufuka na hivyo sisi hatutakufa mauti ya pili. Ni kutegemea yu hai na bado anafanya kazi katika maisha yetu ya kutubadilisha na kututakasa kama sehemu ya wokovu wetu (Flp 1:6, 2:12-13). Ni kutegemea kuna siku atakamilisha wokovu wetu wakati atakaporudi na kubadilisha miili yetu kuwa miili ya utukufu na kutupeleka mbinguni.
Kujumlisha mawazo hayo ya namna ya kuokolewa
Ni muhimu wewe kujikagua na kujiuliza ni aina gani ya imani uliyo nayo.

- Unasema unamwamini Yesu. Je, unaamini Yesu ni Mungu?
- Unasema unamwamini Yesu. Je, umeweka imani yako yote katika yeye bila kuongeza kitu kingine cha pili kama matendo mema n.k.?
- Unasema unamwamini Yesu. Umetubu kweli na kubadilisha mawazo yako kuhusu hali yako ya dhambi na kuhusu Yesu, jinsi alivyo na kazi aliyokufanyia?
- Unasema unamwamini Yesu. Je, unategemea kifo chake kililipa deni la dhambi zako zote, hata zile ambazo bado hujazitenda?
- Unasema unamwamini Yesu. Je, unakubali Yesu ni Bwana na je, imani hiyo imeleta mabadiliko yo yote katika maisha yako kiutendaji?