UINJILISTI UFANYAO KAZI
- 7 -
Kazi za Maombi na Roho Mtakatifu
Huduma ya Uinjilisti inafanyika kwa njia za kimungu. Matokeo yo yote mazuri ni kwa sababu Mungu alisaidia yawepo. Hakuna mwanadamu anayeweza kumshurutisha mtu aokoke. Kwa sababu hiyo ni huduma ambayo lazima ifanywe katika mazingira ya kumwomba Mungu sana. Maombi huonesha kwamba sisi tunajinyenyekeza chini ya uongozi wa Mungu na kumtegemea aifanye kazi yake tukimtumikia.
Tumeshataja katika sura zilizotangulia kwamba mwinjilisti mwenyewe anapaswa kuwa mtu wa maombi. Vilevile tulieleza kwamba timu ya wainjilisti wanapopanga kwenda kushuhudia ni lazima wafanye maombi kwa ajili yao wenyewe pamoja na wale watakaoshuhudiwa.
Zaidi ya hapo kuna njia nyingine ya kutumia maombi inayoleta mafanikio makubwa sana. Njia hiyo ni kutengeneza Orodha ya Maombi ya Uinjilisti.
ORODHA YA MAOMBI YA UINJILISTI NI NINI?
Orodha ya maombi ni orodha maalum ya majina ya watu unaowafahamu na unataka wapate kumpokea Kristo kama Mwokozi wao. Ni orodha ambayo utaitumia kila siku ikukumbushe kuwaombea ukimwomba Mungu kuwaleta kwa Kristo.
KWA NINI NIWE NA ORODHA YA MAOMBI YA UINJILISTI?
Tukio lenye furaha mno linaloweza kutokea kwako kama Mkristo ni kuona mtu unayemfahamu ameupokea wokovu wa Bwana Yesu Kristo. Jambo la kufurahisha zaidi ni kama ulikuwa unamwombea mtu huyu kabla hajampokea Kristo. Katika kitabu kimoja mwandishi Leroy Eims alisema, “Ukitaka kuona watu fulani kuja kwa Kristo, nashauri uyaweke majina yao kwenye orodha ya maombi. Halafu uombe Mungu akupe nafasi za kuwashuhudia ukimwomba vilevile kutayarisha mioyo yao. Uendelee kuomba hadi Mungu atakapotoa jibu lililoahidiwa.” mtume Paulo alionesha moyo wake kwa Waisraeli wenzake katika barua ya Warumi aliposema, “Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe” (Rum. 10:1). Siri ya kupata kuona watu wanakuja kwa Kristo ni kuwaombea na kutaka moyoni mwako waokolewe. Kuwa na “Orodha ya Maombi ya Uinjilisti” kutakusaidia kufanya hivyo.
KUTENGENEZA ORODHA YA MAOMBI YA UINJILISTI
Biblia inasema wazi kwamba, “Bwana...hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba” (2 Pet 3:9). Pia tunayo ahadi kwamba tukiuliza kitu cho chote kulingana na mapenzi ya Mungu, Mungu hutusikia, na hutupa (1 Yoh 5:14-15).
Uinjilisti usiofanyika kwa njia ya maombi huonesha kwamba kazi hii ni ya maarifa na siyo ya kiroho. Lakini tunafahamu kwamba uinjilisti ni huduma ya kiroho siyo ya kimwili. Basi, tufahamu kuwa kazi ya kuokoa watu ni kazi ya Roho Mtakatifu.
KAZI YA ROHO MTAKATIFU KATIKA UINJILISTI
Hakuna anayeweza kuokolewa bila Roho Mtakatifu kumwangaza na kumwonesha hitaji lake la wokovu.
Katika Yohana 16:8-11 Yesu Kristo alieleza kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu kumpatia mpotevu ujumbe wa Neno La Mungu. Roho Mtakatifu hutumia ujumbe wa Neno kuhakikisha juu ya dhambi, haki, na hukumu.
Basi, wajibu wa mwinjilisti ni kupanda mbegu ya Neno la Mungu na kuhakikisha ameipanda vizuri akimwagilia kwa maombi. Kuchipuka na kuota kwa mbegu ni kazi ya Roho Mtakatifu. Wengine wanajivuna kwa kazi zao za uinjilisti wakijaribu kumnyang’anya Roho Mtakatifu kazi na sifa zake. Haiwezikani. Kufanya hivyo ni hatari sana! Kuna hatari aina mbili zinazotokea unapochukua nafasi ya Roho Mtakatifu katika uinjilisti.
Hatari ya kwanza ni kumlazimisha mtu aamini kabla hajafahamu vizuri wala kuwa na moyo uliofunguliwa na Roho Mtakatifu. Yaani, ni kumshawishi msikilizaji kwa maneno mengi au kumgandamiza ili atamke “Sawa nimekubali”, wakati moyo wake ungali haujaamini.
Hatari ya pili ni kujivunia matokeo ya kazi ya uinjilisti. Kufanya hivyo haimpendezi Mungu. Kumbuka Paulo alivyowaelezea Wakorintho, “Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye” (1 Kor 3:6-7). Kumbuka watu wachache wanaokolewa kwa sababu ya kazi ya mwinjilisti mmoja tu.
Kama ndiye Mungu afanyaye kazi hii ya kuokoa, basi tumwachie kazi yake na kuamini Yeye atawaokoa aliowakusudia. Sisi tuendelee kuwa tayari kutumwa naye kama nabii Isaya, “Mimi hapa, nitume mimi!” Tumshukuru na kumsifu Mungu kwa matokeo yoyote katika huduma ya uinjilisti.
MASWALI NA MAJADILIANO
MAZOEZI
Fikiri kuhusu mahitaji ya kila mmoja wa watu wafuatao. Andika mahitaji yao makuu. Halafu fikiri ni kwa njia gani ambayo ungeweza kumshuhudia kwa kumlenga jinsi alivyo; ni sehemu gani ya Wokovu ungekazia?
Yohana - Hana muda wa kwenda kanisani. Anazo shughuli nyingi na kuziacha shughuli zake kutamgharimia kifedha.
Happy - Msichana anayekuwa tayari kusikiliza na kukubali mambo yote bila kutafakari. Anasali na marafiki zake popote wanapopenda.
Albert - Mkristo wa siku nyingi katika kanisa lisilothibitisha wokovu, naye huamini anapoteza wokovu wake anapofanya dhambi. Yaani, hana hakika na wokovu wake.
Neema - Mkristo wa jina tu anayetafuta msaada wa kimwili ndani ya kanisa akitaka faida.
Iddigraf - Msomi mwenye kazi ya kiofisi. Huamini Biblia ni historia tu yenye tafsiri mbalimbali. Huona kwenda kanisani ni kwa maskini na wasio na elimu.
Edigar - Hupenda kuongea Neno la Mungu. Anauliza maswali mengi yasiyohusu Injili na anapenda kujadili na kubishana bila kuamini.

- Mwombe Mungu akupe hekima unapotengeneza orodha yako.
- Jaribu kuorodhesha majina 5 hadi 10 ya watu wasiomwamini Kristo ambao unakutana nao mara kwa mara. Hawa wanaweza kuwa majirani, familia, watu kazini, marafiki shuleni, au wengine. Unaweza kuongeza watu kwenye orodha yako wakati Mungu atakapokukumbushia mtu.
- Tumia karatasi au kadi ndogo kuandika majina haya na uiweke ndani ya Biblia yako ili uione kila mara. Labda utumie kadi hii kama kumbukumbu ya kujisomea Biblia. Anza kutumia kadi au orodha hivi na uwe macho katika kuujenga urafiki na uhusiano na hawa unaowaombea.
Biblia inasema wazi kwamba, “Bwana...hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba” (2 Pet 3:9). Pia tunayo ahadi kwamba tukiuliza kitu cho chote kulingana na mapenzi ya Mungu, Mungu hutusikia, na hutupa (1 Yoh 5:14-15).
Uinjilisti usiofanyika kwa njia ya maombi huonesha kwamba kazi hii ni ya maarifa na siyo ya kiroho. Lakini tunafahamu kwamba uinjilisti ni huduma ya kiroho siyo ya kimwili. Basi, tufahamu kuwa kazi ya kuokoa watu ni kazi ya Roho Mtakatifu.
KAZI YA ROHO MTAKATIFU KATIKA UINJILISTI
Hakuna anayeweza kuokolewa bila Roho Mtakatifu kumwangaza na kumwonesha hitaji lake la wokovu.
Katika Yohana 16:8-11 Yesu Kristo alieleza kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu kumpatia mpotevu ujumbe wa Neno La Mungu. Roho Mtakatifu hutumia ujumbe wa Neno kuhakikisha juu ya dhambi, haki, na hukumu.
Basi, wajibu wa mwinjilisti ni kupanda mbegu ya Neno la Mungu na kuhakikisha ameipanda vizuri akimwagilia kwa maombi. Kuchipuka na kuota kwa mbegu ni kazi ya Roho Mtakatifu. Wengine wanajivuna kwa kazi zao za uinjilisti wakijaribu kumnyang’anya Roho Mtakatifu kazi na sifa zake. Haiwezikani. Kufanya hivyo ni hatari sana! Kuna hatari aina mbili zinazotokea unapochukua nafasi ya Roho Mtakatifu katika uinjilisti.
Hatari ya kwanza ni kumlazimisha mtu aamini kabla hajafahamu vizuri wala kuwa na moyo uliofunguliwa na Roho Mtakatifu. Yaani, ni kumshawishi msikilizaji kwa maneno mengi au kumgandamiza ili atamke “Sawa nimekubali”, wakati moyo wake ungali haujaamini.
Hatari ya pili ni kujivunia matokeo ya kazi ya uinjilisti. Kufanya hivyo haimpendezi Mungu. Kumbuka Paulo alivyowaelezea Wakorintho, “Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye” (1 Kor 3:6-7). Kumbuka watu wachache wanaokolewa kwa sababu ya kazi ya mwinjilisti mmoja tu.
Kama ndiye Mungu afanyaye kazi hii ya kuokoa, basi tumwachie kazi yake na kuamini Yeye atawaokoa aliowakusudia. Sisi tuendelee kuwa tayari kutumwa naye kama nabii Isaya, “Mimi hapa, nitume mimi!” Tumshukuru na kumsifu Mungu kwa matokeo yoyote katika huduma ya uinjilisti.
MASWALI NA MAJADILIANO
- Kwa nini maombi ni lazima katika huduma ya uinjilisti?
- Orodha ya Maombi ya Uinjilisti ni nini? Inasaidia nini?
- Roho Mtakatifu hufanya kazi gani katika uinjilisti?
- Wajibu wetu ni nini katika Uinjilisti?