UINJILISTI UFANYAO KAZI
- 14 -
Mpango Unaohusisha Kanisa Zima
Kwa vile huduma hiyo ya uinjilisti ni muhimu na ni msingi wa kanisa la Mungu lenye uhai, mpango huo ungehusu kanisa zima. Maana, tawi moja la kanisa haliwezi kufaulu kuwatangazia watu wote wa wilaya au mkoa mzima. Basi ni kwa njia gani makanisa yangeweza kushirikiana katika kazi hiyo? Tutumie sura hii ya mwisho kuchunguza vizuri swali hilo na kutoa mapendekezo.
Kwanza kabisa, napenda kukupongeza kwa vile umekisoma kitabu hiki hadi hapa. Maana wewe mwenyewe umejifunza na kujiongezea ujuzi. Zaidi, umeshakuwa mwanga wa kuwafundisha wengine na kuanzisha mpango wa uinjilisti katika tawi lako na katika makanisa mengine yaliyo jirani, Mungu akikujalia. Kitabu hiki kimeandaliwa ili kitumiwe kwa mafundisho na unaweza kukitumia kufundishia semina kwa ajili ya wainjilisti katika mkusanyiko wa matawi mengi au kwa washirika wachache wa tawi lako la mahali.
Paulo alipomfundisha Timotheo alimweleza hivi, “Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine” (2 Tim 2:2). Kwa kweli ni wajibu wako kuyatumia yale uliyojifunza na zaidi kuwakabidhi (kuwafundisha) watu waaminifu wafaao (watakaofanya) ambao watawafundisha na wengine pia. Kwa njia hiyo mambo hayo ya Mungu yataenea kwa nguvu!
Kanisa lenye mpango wa kufundisha uinjilisti kwa washirika wake wote, liteue kundi la wainjilisti wakufunzi. Kanisa, pamoja na wakufunzi hawa, wapange mpango na taratibu za uinjilisti kwa ajili ya makanisa yake. Ndipo wakufunzi hawa watumwe kufundisha wengine katika ngazi mbalimbali kama vile ngazi ya mkoa au senta (yaani uongozi wa huduma za uinjilisti unaohusu mikusanyiko ya matawi zaidi ya moja). Katika kufundisha ngazi hizo, mpango uwekwe kupeleka mafundisho na huduma yenyewe katika kila tawi wakifundisha njia za uinjilisti na wakisimamisha namna huduma itakavyofanyika na jinsi taarifa zitakavyotolewa.
Itasaidia kama makundi ya uinjilisti yataanzishwa katika tawi, senta, na mkoa. Ndani ya makundi haya kamati za unijilisti zingekuwepo za kudumu ili waweze kukutana kila miezi mitatu au nusu mwaka kujengana na kushauriana kuhusu maendeleo na mahitaji ya huduma hiyo. Ingefaa kamati hizo pia zifanye mpango wa kupata mfuko wa fedha kuendeshea shughuli zote za tawi, senta, na mkoa wakitafuta kununua vifaa kama maandiko na vingine. Kamati hizo zikikutana zinaweza kuweka malengo ya uinjilisti katika maeneo yao na pia wanaweza kupanga namna ya kushirikiana katika kulenga vijiji vipya huku wakikumbuka umuhimu wa ufuatiliaji. Hawa vilevile wangeweza kutoa taarifa ya kila mara na kuipeleka kwa mkurugenzi au kamati ya uinjilisti wa kanisa zima.
Kamati hiyo ya uinjilisti wa kanisa zima inahitaji kuwa na wafuatiliaji wa vifaa kama traksi, masomo ya waumini wapya, Biblia na Agano Jipya, na maandiko na masomo mengine.
Muundo mwenyewe wa kushirikiana ungekuwa kama mchoro huu:

Kwa kufuata muundo kama huo, au mwingine unaofanana, kanisa zima linaweza kufaulu zaidi katika kueneza Injili kupitia watu wao. Mpango wao wa kushirikiana utaongeza nguvu na mafanikio yao wakitegemea uongozi na nguvu za Roho Mtakatifu. Vilevile wataweza kupima maendeleo yao na kuboresha taratibu zao kulingana na habari wanazozikusanya.
Makanisa mengi hayana maendeleo kwa vile wameamua uinjilisti ni kazi ya mtu maalum au kundi maalum ndani ya kanisa na siyo huduma ya watu wote kama tulivyojifunza katika kitabu hiki. Mungu hutaka kila Mkristo kulima na kuvuna katika shamba lake. Ndiyo mpango wake wa kuipeleka Injili hadi mwisho wa dunia.
Tuachane na mawazo yanayosema uinjilisti lazima uwe na vyombo na mitambo ya kisasa ya bei ghali. Vyombo vyenyewe sivyo vibaya, tena vinaweza kusaidia uinjilisti. Lakini mawazo yanayosema vyombo ni vya lazima ni kinyume na mpango wa Mungu. Maana, mawazo hayo huathiri watu na kuwafikisha katika wazo la kusema, “Bila vyombo basi hatuwezi kushuhudia.” Yesu Kristo na mitume wake walikuwa vyombo tosha vya uinjilisti. Nasi tuwe vyombo vya Mungu (2 Tim 2:21) tukipeleka Injili duniani pote! Mungu akubariki!
RATIBA YA SEMINA YA SIKU SITA KWA KUTUMIA KITABU HIKI

JUMAPILI - Kuwapitia waumini wapya na kuwapeleka kanisani na kukaa nao. Kushuhudia kanisani ulivyojifunza kwenye semina na kumshukuru Mungu kwa yote.
Vitabu Vilivyonisaidia Kuandika Kitabu Hiki

- Ushuhuda Ufaao na (Evangel Publishing House: Kisumu, Kenya) 1977.
- Uinjilisti wa Maandiko na George Verwer; Operation Mobilization na (nakala ya Kiswahili - Kituo cha Maandiko Habari Maalum: Tabora, TZ) 1985.
- Uvuvi wa Watu na William Macdonald; (Emmaus Bible School: Dar es Salaam, TZ).
- Uinjilisti na D.A. Brown; (Central Tanganyika Press: Dodoma, TZ ) 1967
- Kukua kwa Kanisa na Dr. Vergil Gerber; (Inland Publishers: Mwanza, TZ) 1978.