UINJILISTI UFANYAO KAZI
- 11 -
Kumsaidia Mwongofu Mara Anapokata Shauri
Tunapofanya kazi hatuwezi kufanya bila kutegemea mafanikio. Ni wakulima wangapi wanaoenda shambani na kufanya kazi ya kupanda na kutunza mimea bila kutegemea mavuno? Katika kitabu hiki tunajifunza kuhusu “uinjilisti ufanyao kazi”. Kusudi letu katika kazi ya uinjilisti ni kuona mafanikio au mavuno. Lengo la kuieneza Injili ni kuvuta na kupokea walioandaliwa na Bwana kuingia katika familia yake Mungu.
Kama ndivyo, basi, mwinjilisti anapaswa kufanya nini na yule aliyemshuhudia ambaye yu tayari kukata shauri na kumpokea Kristo kama Bwana na Mwokozi wake. Hapo chini kuna mapendekezo ya mambo muhimu ya kufanya.
1. Omba pamoja naye.
Umsaidie msikilizaji kwa kumwombea ili awe na imani ya kumpokea Kristo na kubadilika. Pia, uwe tayari kumwongoza na maombi ya sala ya toba. Sala ya toba ni nafasi yake kumwambia Mungu hitaji lake la wokovu. Yaani, yeye ni mwenye dhambi, anaungama dhambi zake, na anataka kumwamini Kristo na kazi yake ya ukombozi ili aingie katika familia ya Mungu. Labda utamwongoza kifungu kwa kifungu akikuiga, au akiweza amwelezee Mungu mwenyewe. Mara nyingine unaweza kuonesha sala kama imeandikwa mahali fulani kwenye karatasi.
2. Umpongeze sana kwa uamuzi wa busara na muhimu.
Mtu yule sasa hivi amefaulu mtihani wa maisha yake yote. Amezaliwa upya. Ametoka kifungoni mwa Shetani na kuingia katika uhuru wa Mungu! Huyu anastahili pongezi na anastahili kujua malaika wanasherehekea mbinguni! Uijenge imani yake kwa kuonesha uamuzi wake ni wa maana sana.
3. Umsaidie kifungu angalau kimoja kuhusu “Uhakika wa Wokovu”.
Vifungu ni vingi lakini napendekeza vinne: Yohana 3:16; 5:24; 6:47; au 1 Yohana 5:11-13. Vyote hivi nimevitumia kumhakikishia mwongofu kwamba kitendo chake cha kuamini ndicho kinachookoa na kumpa uzima wa milele.
Kawaida ufungue Biblia na kuisoma pamoja naye. Ni vizuri akisoma mwenyewe. Halafu umwulize maswali kama yafuatayo: (1) Kulingana na Neno La Mungu, Je, ukiamini unapata nini? (2) Kupata uzima wa milele unapaswa kufanya nini? (3) Je, sasa hivi umefanya nini? Umeamini kweli? (4) Basi, kuanzia sasa umepata nini? (5) Unajuaje? (6) Neno la Mungu linakuhakikishaje?
Mwisho, ni vizuri umweleze kwamba Shetani hafurahishwi na uamuzi wake na atajitahidi kutia mashaka juu ya wokovu wake ili asiliamini Neno La Mungu. Lakini umwambie asiyategemee mawazo yake (Mith 3:5, 6) bali ategemee Neno la Mungu.
4. Uhakikishe kwamba anayo Biblia au Agano Jipya.
Unapaswa kumwelezea kuhusu umuhimu wa kulisoma Neno La Mungu ambalo ni chakula chake cha kiroho. Umwambie asome sura moja kila siku akianza na kitabu rahisi kama Injili ya Yohana.
5. Mfundishe kuhusu umuhimu wa kushirikiana kanisani.
Kuni moja au kaa moja haliwezi kuwaka na kuwa moto. Vilevile ni lazima wakristo washirikiane na kujengana kama familia ya Mungu. Umwambie mahali kanisa lako lilipo na ratiba za ibada zake. Pia ufanye mpango wa kuja kumchukua kwenda kanisani Jumapili. Utakapofika kanisani umfahamishe kwa mchungaji, lakini uwe mwangilifu usije ukamwaibisha.
6. Mpatie masomo ya muumini mpya.
Masomo yanayolenga muumini mpya yatamfaa ili aanze kujifunza mara moja. Kama kanisa lako lina vipindi au darasa kwa ajili ya waumini wapya umtaarifu na umsindikize kwenye vipindi hivyo. Masomo yanayofaa ni kama “Hatua za Kukua Kikristo” yanayotolewa na Uinjilisti wa Maandiko (Box 77 Sumbawanga na Box 1745 Mbeya) au “Haya Yote ni Nini” yanatolewa na World Home Bible League (Nairobi) au mengine kwa Life Ministry (Nairobi).
7. Andika jina, anwani, na simu yako na upate jina, anwani, na simu yake.
Hakuna kitu kibaya kama kumwongoza mtu kukata shauri halafu kukosa kumfuatilia. Taarifa kamili ya jina, anwani, na simu itakusaidia kumfuatilia. Pia utaweza kumpa mchungaji au washirika wengine habari hizo ili wamfahamu na kujua anakaa wapi kusudi nao wasaidie katika kumjenga. Usimtambulishe kuwa mwembamba yule mwenye shati nyekundu kidogo.
Mambo haya yote yalioyotajwa hapo juu ni mapendekezo yanayofaa kwa mwongofu mara anapokata shauri. Yaani, siku hiyo hiyo. Katika sura inayofuata tutaangalia jinsi ya kumfuatilia na kumjenga muumini mpya zaidi baada ya siku hiyo kupita.
MASWALI NA MAJADILIANO

- Mtu anaweza kuionesha imani yake na kukata shauri kwa njia gani?
- Vifaa gani vinahitajika kumsaidia mwongofu mara anapokata shauri?
- Unawezaje kumhakikishia mwongofu juu ya wokovu wake?
- Kwa nini kufanya hivyo ni muhimu?
- Ni mambo gani mengine unayopaswa kumfanyia yule anayekata shauri siku hiyo hiyo.
- Andika mfano wa sala ya toba inayoweza kutumiwa na mtu anayetaka kuamini na kuomba.