GMI Publications ni idara ya Grace Ministries International ihusuyo huduma ya vitabu katika lugha ya Kiswahili. Kazi yetu ni kuandika, kuchapisha, na kusambaza vitabu vya Kikristo. Lengo letu ni kusaidia Wakristo kumjua Mungu zaidi, kujenga uhusiano wao naye, na kutimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yao kulingana na mafundisho ya Neno la Mungu.
Kiimani GMI Publications ni Protestanti na Kiuinjilisti (Evangelical).
Misingi mikubwa imani yetu ni kama ifuatayo:
- Tunaamini maneno yote ya Biblia ni yenye pumzi ya Mungu, bila makosa katika nakala za kwanza, na ni mamlaka ya mwisho kuhusu imani yetu na maisha ya Kikristo.
- Tunaamini kuna Mungu mmoja aliye wa milele katika nafsi tatu, Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu.
- Tunaamini Bwana Yesu Kristo ni Mungu 100% na binadamu 100%, alizaliwa na bikira Mariamu, anaishi bila kutenda dhambi, anafanya miujiza, alikufa msalabani badala ya wanadamu wenye dhambi, alifufuka katika mwili wake wa kibinadamu, alipaa kwenda mbinguni kwa mkono wa kulia wa Mungu Baba, na mwenyewe atarudi duniani siku moja katika nguvu na utukufu.
- Tunaamini Mungu anahesabia watu wenye dhambi kuwa wenye haki kwa njia ya neema yake iliyooneshwa wakati Mungu alimtuma Mwana - Bwana Yesu Kristo - kuwa sadaka ya mwenye kumwaga damu yake msalabani na baada ya siku tatu kufufuka. Wokovu huu kamili unatolewa bure na Mungu kama zawadi kwa wote watakaomwamini Yesu Kristo na kazi yake msalabani. Mwanadamu mwenye dhambi hawezi kustahili wokovu huo kupitia jitihada yo yote yake. Ni wale tu wanaomwamini Yesu Kristo ambao wanazaliwa upya na Roho Mtakatifu kuwa watoto wa Mungu.
- Tunaamini Roho Mtakatifu ni Mungu kweli na anafanya kazi ya kuhakikisha wasioamini kuhusu dhambi zao na jinsi walivyo chini ya hukumu ya Mungu, anahuisha mioyo ya wenye dhambi wote wanaomwamini Yesu Kristo, anawabatiza ili waingine katika Mwili wa Kristo, anakaa ndani yao kama ahadi ya wokovu wao, anawatia nuru kuelewa Neno la Mungu, anawawezesha kufanya huduma ya Mungu, na anawawezesha kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu.
- Tunaamini Mungu aliumba mwanaume na mwanamke wa kwanza katika mfano wake, walishindwa kumtii Mungu na hivyo walikufa kiroho na walipewa uwezo wa kufa kimwili. Kama uzao wao, wanadamu wote wanazaliwa na asili ya dhambi na pia wanatenda dhambi, na hawawezi kumpendeza Mungu kwa njia yo yote katika hali hii.
- Tunaamini watu wote waliokufa watafufuliwa kimwili katika siku za mwisho. Wenye imani waliookoka watafufuliwa kuingia utukufu wa milele na wasiookoka kwa ajili ya kuhukumiwa milele.

Proudly powered by Weebly