GMI PUBLICATIONS
GMI PUBLICATIONS
  • Home
  • Kupakua Vitabu
  • Kuhusu Sisi
  • Mawasiliano
  • Home
  • Kupakua Vitabu
  • Kuhusu Sisi
  • Mawasiliano

Ruthu
​(pakua hapo chini)


Picture

Mara kwa mara Wakristo wanajisikia kwamba Mungu amewasahau, hawajali, au hajishughulishi na maisha yao. Kitabu hiki ni somo kwa ajili ya msomaji kujisomesha akijifunza kutoka Biblia yenyewe jinsi Mungu daima anajishughulisha na watu wake. Mfano wa maisha ya Ruthu unafariji Wakristo wote. Isitoshe kitabu hiki kinafundisha jinsi Boazi alivyomkomboa Ruthu na jinsi alivyokuwa mfano wa Yesu ambaye alikuja kukomboa watu wote. Bila historia ya Ruthu tusingeelewa vizuri sababu za Yesu kuja duniani kuwa mwanadamu ili akomboe watu msalabani.

Publisher: GMI Publications
Mwandishi: Dr. William Vinton
Kurasa: 32
​Copyright © 2017
​
PAKUA FAILI YA PDF A4
(Faili hii ni nzuri kwa ajili ya kusoma kwenye kompyuta ama kuprint na kupiga photocopy kwenye karatasi za saizi ya A4) 
PAKUA FAILI YA EPUB
(Faili hii ni nzuri kwa ajili ya kusoma kwenye Simu ama Tablet lakini utahitaji kupakua E-Reader kwanza - Somo maelezo hapo chini)
SOMA BILA KUPAKUA
(Chagua hii ukitaka kusoma kitabu hiki kwenye simu au kompyuta yako bila kupakua ili kisichukue nafasi kwenye simu au kompyuta yako) 
BURE - Vitabu vyetu vyote ni bure kupakua na kutumia kwenye simu au kompyuta yako.

HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA - ​GMI Publications ina haki zote za tafsiri ya kitabu hiki. Hairuhusiwi kuchapa na kuuza sehemu yo yote ya kitabu hiki bila ruhusua ya GMI Publications. Vilevile hairuhusiwi kuuza nakala za kikompyuta (digital copies) bila ruhusa ya GMI Publications

NAMNA YA KUTUMIA - Pengine simu au kompyuta yako tayari inaweza kufungua faili hizo ili uweze kuzisoma. Kama hapana kuna application nyingi unazoweza kupakua bure kwenye intaneti katika "Android Play Store" au "App Store" kwa Apple (iphone huja na "Books App" inayoweza kusoma EPUB). PDF ni vigumu kusoma kwenye simu hivyo ni bora kupakua faili ya EPUB na kupata application (E-READER) inayoweza kusoma EPUB. Mifano ya application za E-READER za kupakua ni "Play Books", au "PocketBook", au "FBReader", au "UB Reader" n.k. Kwa kweli ziko nyingi na unaweza kuchagua application unayotaka mwenyewe. Lazima, tu, application unayochagua iweze kusoma "E-BOOK" ya aina ya EPUB.


Proudly powered by Weebly